Yeremia 4:1-2
Yeremia 4:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ukitaka kurudi ee Israeli, nirudie mimi. Ukiviondoa vitu vya kuchukiza mbele yangu, usipotangatanga huko na huko, ukiapa kwa ukweli, unyofu na uadilifu, kwa kusema, ‘Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo’, ndipo mataifa yatakapopata baraka kwangu, na kutukuka kwa sababu yangu.”
Yeremia 4:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa; nawe utaapa hivi, Kama BWANA aishivyo, katika kweli, na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watabarikiwa na yeye, nao watajitukuza katika yeye.
Yeremia 4:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa; nawe utaapa hivi, Kama BWANA aishivyo, katika kweli, na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watajibariki katika yeye, nao watajitukuza katika yeye.
Yeremia 4:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Ikiwa utataka kurudi, ee Israeli, nirudie mimi,” asema BWANA. “Ikiwa utaondoa sanamu zako za kuchukiza mbele ya macho yangu na usiendelee kutangatanga, ikiwa kwa kweli, kwa haki na kwa unyofu utaapa, ‘Kwa hakika kama vile BWANA aishivyo,’ ndipo mataifa yatakapobarikiwa naye na katika yeye watajitukuza.”