Yohane 16:1-4
Yohane 16:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
“Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu. Watu watawafukuza nyinyi katika masunagogi yao. Tena, wakati unakuja ambapo kila atakayewaua nyinyi atadhani anamhudumia Mungu. Watawatendeeni mambo hayo kwa sababu hawamjui Baba, wala hawanijui mimi. Basi, nimewaambieni mambo haya ili saa yake itakapofika mkumbuke kwamba niliwaambieni. “Sikuwaambieni mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
Yohane 16:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maneno hayo nimewaambia, msije mkakwazwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa inakuja kila mtu awauaye atakapodhania ya kuwa anamfanyia Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi niliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nilikuwapo pamoja nanyi.
Yohane 16:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.
Yohane 16:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani. Watawatenga na masinagogi. Naam, saa yaja ambayo mtu yeyote atakayewaua atadhani kwa kufanya hivyo anamtumikia Mungu. Nao watawatenda haya kwa sababu hawamjui Baba wala mimi. Lakini nimewaambia ninyi mambo haya, ili saa hiyo ikiwadia mpate kukumbuka ya kuwa nilikuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.