Yobu 22:1-11
Yobu 22:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo huyo Elifazi Mtemani akajibu, na kusema, Je! Yumkini mtu awaye yote kumfaa Mungu? Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe. Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu? Je! Ni kwa wewe kumcha yeye anakukemea? Na kuingia hukumuni nawe? Je! Uovu wako si mkuu? Wala maovu yako hayana mwisho. Kwa kuwa umetwaa dhamana kwa nduguyo bure, Na kuwavua nguo zao walio uchi. Hukumpa maji ya kunywa huyo aliyechoka, Nawe umemnyima chakula huyo mwenye njaa. Lakini huyo shujaa, nchi ilikuwa yake; Na huyo mwenye kusifiwa, yeye aliikaa. Umewafukuza wanawake wajane hali ya utupu, Na mikono ya mayatima imevunjwa. Kwa hiyo umezungukwa na mitego, Na hofu ya ghafula yakutaabisha, Au je! Huoni giza, Na maji mengi yanayokufunika?
Yobu 22:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Elifazi, Mtemani, akajibu Yobu: “Je, binadamu anafaa chochote kwa Mungu? Kwa kweli mwenye hekima anajifaidi mwenyewe tu. Je, unadhani wamfurahisha Mungu kwa kuwa mnyofu? Au anapata faida gani kama huna hatia? Unadhani anakurudi na kukuhukumu kwa sababu wewe unamheshimu? La! Uovu wako ni mkubwa mno! Ubaya wako hauna mwisho! Wewe umemnyanganya ndugu yako nguo ya rehani; umemchukulia nguo hiyo moja aliyokuwa nayo. Umewanyima maji wale waliokuwa wamechoka; umewanyima chakula wale walio na njaa. Umemruhusu mwenye cheo kuchukua ardhi yote; umemwacha anayependelewa aishi humo. Umewaacha wajane waende mikono mitupu; umewanyima yatima uwezo wao. Kwa hiyo mitego imekuzunguka pande zote, hofu ya ghafla imekuvamia. Giza limekuangukia usione kitu; mafuriko ya maji yamekufunika.
Yobu 22:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo huyo Elifazi Mtemani akajibu, na kusema, Je! Yumkini mtu awaye yote kumfaa Mungu? Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe. Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu? Je! Ni kwa wewe kumcha yeye anakukemea? Na kuingia hukumuni nawe? Je! Uovu wako si mkuu? Wala maovu yako hayana mwisho. Kwa kuwa umetwaa dhamana kwa nduguyo bure, Na kuwavua nguo zao walio uchi. Hukumpa maji ya kunywa huyo aliyechoka, Nawe umemnyima chakula huyo mwenye njaa. Lakini huyo shujaa, nchi ilikuwa yake; Na huyo mwenye kusifiwa, yeye aliikaa. Umewafukuza wanawake wajane bila chochote, Na mikono ya mayatima imevunjwa. Kwa hiyo umezungukwa na mitego, Na hofu ya ghafla yakutaabisha, Au je! Huoni giza, Na maji mengi yanayokufunika?
Yobu 22:1-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo Elifazi Mtemani akajibu: “Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu? Je, hata mtu mwenye hekima aweza kumfaidi? Je, Mwenyezi angefurahia nini kama ungekuwa mwadilifu? Au je, yeye angepata faida gani kama njia zako zingekuwa kamilifu? “Je, ni kwa ajili ya utaua wako ndiyo maana anakukemea na kuleta mashtaka dhidi yako? Je, uovu wako si mkuu? Dhambi zako si hazina mwisho? Umedai dhamana kwa ndugu zako bila sababu; umewavua watu nguo zao, ukawaacha uchi. Hukumpa maji aliyechoka, nawe ulimnyima chakula mwenye njaa, ingawa ulikuwa mtu mwenye uwezo ukimiliki nchi: mtu uliyeheshimiwa, ukiishi ndani yake. Umewafukuza wajane mikono mitupu na kuzivunja nguvu za yatima. Ndiyo sababu mitego imekuzunguka pande zote, hatari ya ghafula inakutia hofu, ndiyo sababu ni giza sana huwezi kuona, tena ndiyo sababu mafuriko ya maji yamekufunika.