Yobu 34:31-37
Yobu 34:31-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwani kuna mtu aliyemwambia Mungu, Mimi nimevumilia kurudiwa, ingawa sikukosa; Nisiyoyaona nifundishe wewe; Kama nimefanya uovu sitafanya tena? Je! Malipo yake yatakuwa kama upendavyo wewe, hata ukayakataa? Kwani yakupasa wewe kuchagua, si mimi; Kwa sababu hiyo sema uyajuayo. Watu walio na akili wataniambia, Naam, kila mtu mwenye hekima anisikiaye; Huyo Ayubu amesema pasipo maarifa, Na maneno yake hayana hekima. Laiti Ayubu angejaribiwa hata mwisho, Kwa kuwa amejibu kama watu waovu. Kwani huongeza uasi juu ya dhambi zake, Apiga makofi kati yetu, Na kuongeza maneno yake kinyume cha Mungu.
Yobu 34:31-37 Biblia Habari Njema (BHN)
“Tuseme mtu amemwambia Mungu, ‘Nimekosa, sitatenda dhambi tena. Nioneshe makosa nisiyoweza kuyaona kama nimetenda mabaya sitayarudia tena.’ Je, Mungu atapaswa kumwadhibu kama uonavyo wewe? Wewe ndiwe unayeamua, sio mimi. Basi, sema unachofikiri wewe. Mtu yeyote mwenye akili, na kila mwenye hekima anayenisikiliza atasema: ‘Yobu anaongea bila kutumia akili, maneno yake hayana maana.’ Laiti Yobu angechunguzwa mpaka mwisho, kwa maana anajibu kama watu waovu. Huongeza uasi juu ya dhambi zake; anaeneza mashaka kati yetu, na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”
Yobu 34:31-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwani kuna mtu aliyemwambia Mungu, Mimi nimevumilia kurudiwa, ingawa sikukosa; Nisiyoyaona nifundishe wewe; Kama nimefanya uovu sitafanya tena? Je! Malipo yake yatakuwa kama upendavyo wewe, hata ukayakataa? Kwani yakupasa wewe kuchagua, si mimi; Kwa sababu hiyo sema uyajuayo. Watu walio na akili wataniambia, Naam, kila mtu mwenye hekima anisikiaye; Huyo Ayubu amesema pasipo maarifa, Na maneno yake hayana hekima. Laiti Ayubu angejaribiwa hadi mwisho, Kwa kuwa amejibu kama watu waovu. Maana huongeza uasi juu ya dhambi zake, Apiga makofi kati yetu, Na kuongeza maneno yake kinyume cha Mungu.
Yobu 34:31-37 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Kama mwanadamu akimwambia Mungu, ‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena. Nifundishe nisichoweza kuona; kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’ Je basi, Mungu atakulipa kwa masharti yako, wakati wewe umekataa kutubu? Yakupasa wewe uamue, wala si mimi; sasa niambie lile ulijualo. “Wanadamu wenye ufahamu husema, wenye hekima wanaonisikia huniambia, ‘Ayubu huongea bila maarifa; maneno yake hayana busara.’ Laiti Ayubu angejaribiwa hadi kikomo cha mwisho, kwa sababu anajibu kama mtu mwovu! Kwenye dhambi yake huongeza uasi; kwa dharau hupiga makofi miongoni mwetu, na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”