Yobu 4:4-6
Yobu 4:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge. Lakini sasa haya yamekufikia wewe, nawe wafa moyo; Yamekugusa, nawe wafadhaika. Je! Dini yako siyo tegemeo lako? Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?
Yobu 4:4-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa; umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu. Lakini sasa hii taabu imekujia wewe, nawe unashuka moyo; imekupiga wewe, nawe unafadhaika. Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa ndiyo matumaini yako na njia zako kutokuwa na lawama ndilo taraja lako?
Yobu 4:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Maneno yako yamewainua waliokufa moyo, umewaimarisha waliokosa nguvu. Lakini sasa yamekupata, nawe ukakosa subira, yamekugusa, nawe ukafadhaika. Je, kumcha Mungu si ndilo tegemeo lako? Na unyofu wako si ndilo tumaini lako?
Yobu 4:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge. Lakini sasa haya yamekufikilia wewe, nawe wafa moyo; Yamekugusa, nawe wafadhaika. Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?