Yobu 41:1-11
Yobu 41:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)
“Yeyote anayeliona hilo dude, hufa moyo na kuzirai. Hakuna mtu yeyote mkali athubutuye kulishtua. Nani, basi awezaye kusimama mbele yangu? Nani aliyenipa kitu, ili nitakiwe kumrudishia? Chochote kilicho chini ya mbingu ni changu. “Sitaacha kukueleza juu ya viungo vya hilo dude au juu ya nguvu zake na umbo lake zuri. Nani awezaye kumbambua vazi lake la nje? Nani awezaye kutoboa deraya lililovaa? Nani awezaye kufungua kinywa chake? Meno yake pande zote ni kitisho! Mgongo wake umefanywa kwa safu za ngao zilizoshikamana pamoja kama kwa mhuri, Kila moja imeshikamana na nyingine, hata hewa haiwezi kupenya katikati yake. Yameunganishwa pamoja, hata haiwezekani kuyatenganisha. Likipiga chafya, mwanga huchomoza, macho yake humetameta kama jua lichomozapo. Kinywani mwake hutoka mienge iwakayo, cheche za moto huruka nje.
Yobu 41:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba? Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu? Je! Atakusihi sana? Au, atakuambia maneno ya upole? Je! Atafanya agano pamoja nawe, Umtwae kuwa mtumishi wako milele? Je! Utamchezea kama ndege? Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako? Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara? Watamgawanya kati ya wafanyao biashara? Je! Waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha, Au kichwa chake kwa vyusa? Mwekee mkono wako; Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena. Tazama, kumtamani ni bure; Je! Hatambwaga chini huyo atakayemtazama? Hapana aliye mkali hata akathubutu kumwamsha; Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi? Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.
Yobu 41:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba? Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu? Je! Atakusihi sana? Au, atakuambia maneno ya upole? Je! Atafanya agano pamoja nawe, Umtwae kuwa mtumishi wako milele? Je! Utamchezea kama ndege? Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako? Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara? Watamgawanya kati ya wafanyao biashara? Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha, Au kichwa chake kwa vyusa? Mwekee mkono wako; Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena. Tazama, kumtamani ni bure; Je! Hatambwaga chini huyo atakayemtazama? Hapana aliye mkali hata akathubutu kumwamsha; Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi? Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.
Yobu 41:1-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Je, waweza kumvua Lewiathani kwa ndoano ya samaki, au kufunga ulimi wake kwa kamba? Waweza kupitisha kamba puani mwake, au kutoboa taya lake kwa kulabu? Je, ataendelea kukuomba umhurumie? Atasema nawe maneno ya upole? Je, atafanya agano nawe ili umtwae awe mtumishi wako maisha yake yote? Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege, au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako? Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake? Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara? Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali, au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki? Kama ukiweka mkono wako juu yake, utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena! Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya; kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini. Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza. Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu? Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa? Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.