Yobu 8:5-7
Yobu 8:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama utamtafuta Mungu ukamsihi huyo Mungu mwenye nguvu, kama wewe u safi moyoni na mnyofu, kweli Mungu atakuja kukusaidia, na kukujalia makao unayostahili. Na ingawa ulianza kuishi kwa unyonge maisha yako ya baadaye yatakuwa ya fahari zaidi.
Yobu 8:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; Ikiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa. Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.
Yobu 8:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa. Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.
Yobu 8:5-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini ukimtafuta Mungu, nawe ukamsihi Mwenyezi, ikiwa wewe ni safi na mnyofu, hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako, na kukurudisha katika mahali pako pa haki. Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo, lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio.