Yoeli 1:13
Yoeli 1:13 Biblia Habari Njema (BHN)
Enyi makuhani, jivikeni magunia kuomboleza, lieni enyi wahudumu wa madhabahu. Ingieni hekaluni mkaomboleze usiku kucha! Sadaka za nafaka na kinywaji zimetoweka nyumbani kwa Mungu.
Yoeli 1:13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njooni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.
Yoeli 1:13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njoni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.
Yoeli 1:13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Vaeni nguo ya gunia, enyi makuhani, muomboleze; pigeni yowe, enyi mnaohudumu madhabahuni. Njooni, vaeni nguo ya gunia usiku kucha, enyi mnaohudumu mbele za Mungu wangu; kwa kuwa sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji zimezuiliwa kufika katika nyumba ya Mungu wenu.