Yona 3:1-5
Yona 3:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Neno la Mwenyezi-Mungu likamjia Yona mara ya pili: “Nenda Ninewi, ule mji mkuu, ukawatangazie watu ujumbe niliokupa.” Basi, Yona akaondoka, akaenda Ninewi kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza. Mji wa Ninewi ulikuwa mkubwa sana. Upana wake ulikuwa mwendo wa siku tatu. Alipowasili, Yona aliingia mjini, na baada ya kutembea mwendo wa siku nzima, akaanza kutangaza: “Bado siku arubaini tu na mji huu wa Ninewi utaangamizwa!” Basi, watu wa Ninewi wakauamini ujumbe wa Mungu, wakatangaza mfungo, na kwamba kila mmoja wao, mkubwa kwa mdogo, avae vazi la gunia kama ishara ya kutubu.
Yona 3:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake ni mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arubaini Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamwamini Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, kuanzia yeye aliye mkubwa hadi aliye mdogo.
Yona 3:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.
Yona 3:1-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili: “Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.” Yona akalitii neno la BWANA naye akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka. Siku ya kwanza, Yona aliingia mjini. Akatangaza: “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.” Watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa nguo za gunia.