Maombolezo 3:1-20
Maombolezo 3:1-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi ni mtu niliyepata mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake Mungu. Amenichukua akanipeleka mpaka gizani kusiko na mwanga. Amenyosha mkono wake dhidi yangu mimi tu, akanichapa tena na tena mchana kutwa. Amenichakaza ngozi na nyama, mifupa yangu ameivunja. Amenizingira na kunizungushia uchungu na mateso. Amenikalisha gizani kama watu waliokufa zamani. Amenizungushia ukuta nisitoroke, amenifunga kwa minyororo mizito. Ingawa naita na kulilia msaada anaizuia sala yangu isimfikie. Njia zangu ameziziba kwa mawe makubwa amevipotosha vichochoro vyangu. Yeye ni kama dubu anayenivizia; ni kama simba aliyejificha. Alinifukuza njiani mwangu, akanilemaza na kuniacha mkiwa. Aliuvuta upinde wake, akanilenga mshale wake. Alinichoma moyoni kwa mishale, kutoka katika podo lake. Nimekuwa kitu cha dhihaka kwa watu wote, mchana kutwa nimekuwa mtu wa kuzomewa. Amenijaza taabu, akanishibisha uchungu. Amenisagisha meno katika mawe, akanifanya nigaegae majivuni. Moyo wangu haujui tena amani, kwangu furaha ni kitu kigeni. Nimewaza “Nimekata tamaa kabisa, tumaini langu kwa Mwenyezi-Mungu limetoweka.” Kukumbuka taabu na kutangatanga kwangu kwanipa uchungu kama wa nyongo. Nayafikiria hayo daima, nayo roho yangu imejaa majonzi.
Maombolezo 3:1-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi ni mtu aliyeona mateso Kwa fimbo ya ghadhabu yake. Ameniongoza na kunipeleka katika giza Wala si katika nuru. Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote. Amechakaza ngozi yangu na nyama yangu; Ameivunja mifupa yangu. Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha uchungu na uchovu. Amenikalisha penye giza, Kama watu waliokufa zamani. Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka; Amenifunga kwa mnyororo mzito. Naam, nikilia na kuomba msaada, Huyapinga maombi yangu. Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa; Ameyapotosha mapito yangu. Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye, Kama simba aliye mafichoni. Amezigeuza njia zangu, na kuniraruararua; Amenifanya ukiwa. Ameupinda upinde wake, Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale. Amenichoma viuno Kwa mishale ya podo lake. Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote; Wimbo wao mchana kutwa. Amenijaza uchungu, Amenikinaisha kwa pakanga. Amenivunja meno kwa changarawe; Amenifunika majivu. Umeniweka nafsi yangu mbali na amani; Nikasahau kufanikiwa. Nikasema, Nguvu zangu zimepotea, Na tumaini langu kwa BWANA. Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo. Nafsi yangu ingali ikiyakumbuka hayo, Nayo imeinama ndani yangu.
Maombolezo 3:1-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi ni mtu aliyeona mateso Kwa fimbo ya ghadhabu yake. Ameniongoza na kuniendesha katika giza Wala si katika nuru. Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote. Amechakaza nyama yangu na ngozi yangu; Ameivunja mifupa yangu. Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha uchungu na uchovu. Amenikalisha penye giza, Kama watu waliokufa zamani. Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka; Ameufanya mnyororo wangu mzito. Naam, nikilia na kuomba msaada, Huyapinga maombi yangu. Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa; Ameyapotosha mapito yangu. Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye, Kama simba aliye mafichoni. Amezigeuza njia zangu, na kunirarua-rarua; Amenifanya ukiwa. Ameupinda upinde wake, Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale. Amenichoma viuno Kwa mishale ya podo lake. Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote; Wimbo wao mchana kutwa. Amenijaza uchungu, Amenikinaisha kwa pakanga. Amenivunja meno kwa changarawe; Amenifunika majivu. Umeniweka nafsi yangu mbali na amani; Nikasahau kufanikiwa. Nikasema, Nguvu zangu zimepotea, Na tumaini langu kwa BWANA. Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo. Nafsi yangu ikali ikiyakumbuka hayo, Nayo imeinama ndani yangu.
Maombolezo 3:1-20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mimi ndiye mtu aliyeona mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake. Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee gizani wala si katika nuru; hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa. Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa na ameivunja mifupa yangu. Amenizingira na kunizunguka kwa uchungu na taabu. Amenifanya niishi gizani kama wale waliokufa. Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, amenifunga kwa minyororo mizito. Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada, anakataa kupokea maombi yangu. Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe, amepotosha njia zangu. Kama dubu aviziaye, kama simba mafichoni, ameniburuta kutoka njia, akanirarua na kuniacha bila msaada. Amevuta upinde wake na kunifanya mimi niwe lengo kwa ajili ya mishale yake. Alinichoma moyo wangu kwa mishale iliyotoka kwenye podo lake. Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote, wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa. Amenijaza kwa majani machungu na kunishibisha kwa nyongo. Amevunja meno yangu kwa changarawe, amenikanyagia mavumbini. Amani yangu imeondolewa, nimesahau kufanikiwa ni nini. Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondoka na yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa BWANA.” Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu, uchungu na nyongo. Ninayakumbuka vyema, nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu.