Maombolezo 3:21-33
Maombolezo 3:21-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye. BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu. Ni vema mwanadamu aichukue nira Wakati wa ujana wake. Na akae peke yake na kunyamaza kimya; Kwa sababu Bwana ameweka hayo juu yake. Na atie kinywa chake mavumbini; Ikiwa yamkini liko tumaini. Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake; Ashibishwe mashutumu. Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.
Maombolezo 3:21-33 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hata hivyo najikumbusha neno hili na kwa hiyo ninalo tumaini. Kwa sababu ya upendo mkuu wa BWANA, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu. Nimeiambia nafsi yangu, “BWANA ni fungu langu, kwa hiyo nitamngojea.” BWANA ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake, kwa yule ambaye humtafuta; ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa BWANA. Ni vyema mtu kuchukua nira bado angali kijana. Na akae peke yake awe kimya, kwa maana BWANA ameiweka juu yake. Na azike uso wake mavumbini bado panawezekana kuwa na matumaini. Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, na ajazwe na aibu. Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali na Bwana milele. Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma, kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu. Kwa maana hapendi kuwaletea mateso au huzuni watoto wa wanadamu.
Maombolezo 3:21-33 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini nakumbuka jambo hili moja, nami ninalo tumaini: Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno. Mwenyezi-Mungu ndiye hazina yangu hivyo nitamwekea tumaini langu. Mwenyezi-Mungu ni mwema kwa wanaomtegemea, ni mwema kwa wote wanaomtafuta. Ni vema mtu kungojea kwa saburi ukombozi utokao kwa Mwenyezi-Mungu. Ni vema mtu kujifunza uvumilivu tangu wakati wa ujana wake. Heri kukaa peke na kimya, mazito yanapompata kutoka kwa Mungu. Yampasa kuinama na kujinyenyekesha, huenda ikawa tumaini bado lipo. Yampasa kumgeuzia shavu mwenye kumpiga, na kuwa tayari kupokea matusi yake. Mwenyezi-Mungu hatatutupa milele. Ingawa atufanya tuhuzunike, atakuwa na huruma tena kadiri ya wingi wa fadhili zake. Yeye hapendelei kuwatesa wala kuwahuzunisha wanadamu.
Maombolezo 3:21-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)