Luka 14:28-30
Luka 14:28-30 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.
Luka 14:28-30 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia? La sivyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, watu watamcheka wakisema: ‘Mtu huyu alianza kujenga, lakini hakumalizia.’
Luka 14:28-30 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, haketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.
Luka 14:28-30 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha? La sivyo, akiisha kuweka msingi, naye akiwa hana uwezo wa kuikamilisha, wote waionao wataanza kumdhihaki, wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini hakuweza kukamilisha.’