Mathayo 14:18-19
Mathayo 14:18-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu akawaambia, “Nileteeni hapa.” Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.
Mathayo 14:18-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akasema, Nileteeni hapa. Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano.
Mathayo 14:18-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.” Yesu akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano.
Mathayo 14:18-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)