Nehemia 9:16-17
Nehemia 9:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wao na babu zetu wakawa na kiburi na wakawa na shingo ngumu wakakataa kufuata maagizo yako. Wakakataa kutii; wasiyakumbuke maajabu uliyofanya miongoni mwao. Wakawa na shingo zao ngumu, wakajichagulia kiongozi wa kuwarudisha utumwani nchini Misri. Bali wewe Mungu u mwepesi kusamehe, mwenye neema na huruma, wewe hukasiriki upesi. U mwenye fadhili nyingi, na hukuwatupa.
Nehemia 9:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini wao na baba zetu wakatakabari, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wala hawakuzisikiliza amri zako, ila wakakataa kutii, wala hawakuyakumbuka maajabu yako, uliyoyafanya kati yao; lakini wakafanya shingo zao kuwa ngumu, na katika kuasi kwao wakaweka jemadari, ili wairudie hali ya utumwa; lakini wewe u Mungu, uliye tayari kusamehe, mwenye neema, mwenye huruma nyingi, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, basi hukuwaacha.
Nehemia 9:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini wao na baba zetu wakatakabari, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wala hawakuzisikiliza amri zako, ila wakakataa kutii, wala hawakuyakumbuka maajabu yako, uliyoyafanya kati yao; lakini wakafanya shingo zao kuwa ngumu, na katika kuasi kwao wakaweka jemadari, ili wairudie hali ya utumwa; lakini wewe u Mungu, uliye tayari kusamehe, mwenye neema, mwenye huruma nyingi, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, basi hukuwaacha.
Nehemia 9:16-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Lakini wao, baba zetu, wakawa na kiburi na shingo ngumu, nao hawakutii maagizo yako. Wakakataa kusikiliza na kushindwa kukumbuka miujiza uliyoifanya miongoni mwao. Wakawa na shingo ngumu, na katika uasi wao wakamchagua kiongozi ili warudi kwenye utumwa wao. Lakini wewe ni Mungu mwenye kusamehe, mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo. Kwa hiyo hukuwaacha