Nehemia 9:19-21
Nehemia 9:19-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Wewe kwa huruma zako nyingi hukuwatupa kule jangwani. Mnara wa wingu uliowaongoza mchana haukuondoka, wala mnara wa moto uliowamulikia njia usiku, haukuondoka. Ukawapa roho yako njema kuwashauri; ukawapa mana kuwa chakula chao na maji ya kunywa ili kutuliza kiu chao. Ukawatunza jangwani kwa miaka arubaini na hawakukosa chochote; mavazi yao hayakuchakaa wala nyayo zao hazikuvimba.
Nehemia 9:19-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
hata hivyo wewe kwa wingi wa rehema zako hukuwaacha jangwani; nguzo ya wingu haikuondoka kwao wakati wa mchana, ili kuwaongoza njiani; wala nguzo ya moto haikuondoka wakati wa usiku, ili kuwapa mwanga na kuwaonesha njia watakayoiendea. Ukawapa na roho yako mwema ili kuwaelimisha, wala hukuwanyima mana vinywani mwao, tena ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao. Naam, muda wa miaka arubaini uliwaruzuku jangwani, wasihitaji kitu; nguo zao hazikuchakaa, wala miguu yao haikuvimba.
Nehemia 9:19-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
hata hivyo wewe kwa wingi wa rehema zako hukuwaacha jangwani; nguzo ya wingu haikuwaondokea wakati wa mchana, ili kuwaongoza njiani; wala nguzo ya moto haikuondoka wakati wa usiku, ili kuwapa mwanga na kuwaonyesha njia watakayoiendea. Ukawapa na roho yako mwema ili kuwaelimisha, wala hukuwanyima mana vinywani mwao, tena ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao. Naam, muda wa miaka arobaini uliwaruzuku jangwani, wasihitaji kitu; nguo zao hazikuchakaa, wala miguu yao haikuvimba.
Nehemia 9:19-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Kwa sababu ya huruma zako kuu hukuwaacha jangwani. Wakati wa mchana ile nguzo ya wingu haikukoma kuwaongoza katika njia yao, wala nguzo ya moto haikuacha kuwamulikia usiku njia iliyowapasa kuiendea. Uliwapa Roho wako mwema ili kuwafundisha. Hukuwanyima mana yako vinywani mwao, nawe ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao. Kwa miaka arobaini uliwatunza jangwani. Hawakukosa chochote, na nguo zao hazikuchakaa wala miguu yao haikuvimba.