Methali 1:1-7
Methali 1:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na tahadhari; mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia. Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao. Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Methali 1:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Hizi ni methali za Solomoni mfalme wa Israeli, mwana wa Daudi. Methali hizi zawapatia watu hekima na nidhamu; zawafanya waelewe maneno ya busara, zawafanya kuwa na nidhamu, utaratibu, uadilifu, haki na kutenda kwa usawa. Huwapatia wajinga werevu na vijana maarifa na hadhari. Mwenye hekima azisikie na kuongeza elimu yake, naye mwenye busara apate mwongozo. Mtu aelewe methali na mifano, maneno ya wenye hekima na vitendawili vyao. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Methali 1:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari; mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia. Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao. Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Methali 1:1-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli: Kwa kupata hekima na nidhamu; kwa kufahamu maneno ya busara; kwa kujipatia nidhamu na busara, kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea; huwapa busara wajinga, maarifa na akili kwa vijana; wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao, wenye kupambanua na wapate mwongozo; kwa kufahamu mithali na mifano, misemo na vitendawili vya wenye hekima. Kumcha BWANA ndicho chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.