Methali 1:2-5
Methali 1:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Methali hizi zawapatia watu hekima na nidhamu; zawafanya waelewe maneno ya busara, zawafanya kuwa na nidhamu, utaratibu, uadilifu, haki na kutenda kwa usawa. Huwapatia wajinga werevu na vijana maarifa na hadhari. Mwenye hekima azisikie na kuongeza elimu yake, naye mwenye busara apate mwongozo.
Methali 1:2-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na tahadhari; mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
Methali 1:2-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari; mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
Methali 1:2-5 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kwa kupata hekima na nidhamu; kwa kufahamu maneno ya busara; kwa kujipatia nidhamu na busara, kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea; huwapa busara wajinga, maarifa na akili kwa vijana; wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao, wenye kupambanua na wapate mwongozo