Methali 27:8-14
Methali 27:8-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtu aliyepotea mbali na kwake, ni kama ndege aliyepotea mbali na kiota chake. Mafuta na manukato huufurahisha moyo, lakini taabu hurarua roho. Usisahau rafiki zako wala wa baba yako. Ukipatwa na janga usikimbilie kwa nduguyo; afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali. Uwe na hekima mwanangu upate kunifurahisha moyo, nami sitakosa la kumjibu yeyote anayenilaumu. Mwenye busara huona hatari akajificha, lakini mjinga hujitokeza mbele akaumia. Mtu akiahidi mbele yako kumdhamini mgeni, chukua nguo yake; mfanye awajibike kwa kuwadhamini wageni. Amwamkiaye jirani kwa kelele alfajiri, itaeleweka kwamba amemtakia laana.
Methali 27:8-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama ndege aendaye huku na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huku na huko mbali na mahali pake. Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake. Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali. Mwanangu, uwe na hekima na kunifurahisha moyo wangu; Ili nipate kumjibu anilaumuye. Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni; Mtoza rehani aliye mdhamini wa malaya. Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.
Methali 27:8-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake, ndivyo alivyo mtu atangatangaye mbali na nyumbani mwake. Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, nao uzuri wa rafiki huchipuka kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu. Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, tena usiende nyumbani mwa ndugu yako wakati umepatwa na maafa. Bora jirani wa karibu kuliko ndugu aliye mbali. Mwanangu, uwe na hekima, nawe ulete furaha moyoni mwangu, ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote anitendaye kwa dharau. Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa. Chukua vazi la yule awekaye dhamana kwa ajili ya mgeni; lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo kwa ajili ya mwanamke mpotovu. Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu asubuhi na mapema, itahesabiwa kama ni laana.
Methali 27:8-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama ndege aendaye huko na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huko na huko mbali na mahali pake. Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake. Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali. Mwanangu, uwe na hekima na kunifurahisha moyo wangu; Ili nipate kumjibu anilaumuye. Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni; Mtoza rehani aliye mdhamini wa malaya. Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.