Methali 3:13-15
Methali 3:13-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Heri mtu yule aonaye hekima, mtu yule apataye ufahamu, kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi. Hekima ana thamani kuliko marijani; hakuna chochote unachokitamani kinachoweza kulinganishwa naye.
Methali 3:13-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Heri mtu anayegundua hekima, mtu yule anayepata ufahamu. Hekima ni bora kuliko fedha, ina faida kuliko dhahabu. Hekima ina thamani kuliko johari, hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo.
Methali 3:13-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.
Methali 3:13-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)