Methali 6:16-19
Methali 6:16-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia, moyo uwazao mipango miovu, miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu, shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo, na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.
Methali 6:16-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Kuna vitu sita anavyochukia Mwenyezi-Mungu; naam, vitu saba ambavyo ni chukizo kwake: Macho ya kiburi, ulimi mdanganyifu, mikono inayoua wasio na hatia, moyo unaopanga mipango miovu, miguu iliyo mbioni kutenda maovu, shahidi wa uongo abubujikaye uongo, na mtu achocheaye fitina kati ya ndugu.
Methali 6:16-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
Methali 6:16-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)