Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 8:1-21

Methali 8:1-21 Biblia Habari Njema (BHN)

Sikilizeni! Hekima anaita! Busara anapaza sauti yake! Juu penye mwinuko karibu na njia, katika njia panda ndipo alipojiweka. Karibu na malango ya kuingilia mjini, mahali wanapoingia watu anaita kwa sauti: “Enyi watu wote, nawaita nyinyi! Wito wangu ni kwa ajili ya binadamu. Enyi wajinga, jifunzeni kuwa na akili; sikilizeni kwa makini enyi wapumbavu. Sikilizeni maana nitakachosema ni jambo muhimu; midomoni mwangu mtatoka mambo ya adili. Kinywa changu kitatamka kweli tupu; uovu ni chukizo midomoni mwangu. Kinywa changu kitatamka maneno ya kweli, udanganyifu ni haramu midomoni mwangu. Kwa mtu mwelewa kila kitu ni wazi, kwa mwenye maarifa yote ni sawa. Chagua mafundisho yangu badala ya fedha; na maarifa badala ya dhahabu safi. “Mimi Hekima nina thamani kuliko johari; chochote unachotamani hakiwezi kulingana nami. Mimi Hekima ninao ujuzi; ninayo maarifa na busara. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni kuchukia uovu. Nachukia kiburi, majivuno na maisha mabaya; nachukia na lugha mbaya. Nina uwezo wa kushauri na nina hekima. Ninao ujuzi na nina nguvu. Kwa msaada wangu wafalme hutawala, watawala huamua yaliyo ya haki. Kwa msaada wangu viongozi hutawala, wakuu na watawala halali. Nawapenda wale wanaonipenda; wanaonitafuta kwa bidii hunipata. Utajiri na heshima viko kwangu, mali ya kudumu na fanaka. Matunda yangu ni mazuri kuliko dhahabu safi, faida yangu yashinda ile ya fedha bora. Natembea katika njia ya uadilifu; ninafuata njia za haki. Mimi huwatajirisha wanaonipenda, huzijaza tele hazina zao wanipendao.

Shirikisha
Soma Methali 8

Methali 8:1-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake? Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, Penye njia panda, ndipo asimamapo. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele. Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu. Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu. Sikilizeni, maana nitasema yaliyo mazuri, Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili. Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu. Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi. Yote humwelea yule afahamuye, Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa. Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, Na maarifa kuliko dhahabu safi. Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo. Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa makao yangu; Natafuta maarifa na busara. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia. Ushauri ni wangu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu. Kwa msaada wangu wafalme humiliki, Na wakuu wanahukumu haki. Kwa msaada wangu wakuu hutawala, Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia. Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu ni bora kuliko dhahabu, naam, dhahabu safi, Na faida yangu ni bora kuliko fedha iliyo safi. Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao.

Shirikisha
Soma Methali 8

Methali 8:1-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake? Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, Penye njia panda, ndipo asimamapo. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele. Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu. Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu. Sikieni, maana nitasema yaliyo mazuri, Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili. Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu. Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi. Yote humwelea yule afahamuye, Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa. Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, Na maarifa kuliko dhahabu safi. Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo. Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu; Natafuta maarifa na busara. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia. Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu. Kwa msaada wangu wafalme humiliki, Na wakuu wanahukumu haki. Kwa msaada wangu wakuu hutawala, Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia. Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, Na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao.

Shirikisha
Soma Methali 8

Methali 8:1-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Je, hekima haitani? Je, ufahamu hapazi sauti? Juu ya miinuko karibu na njia, penye njia panda, ndipo asimamapo; kando ya malango yaelekeayo mjini, kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema: “Ni ninyi wanaume, ninaowaita; ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote. Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili; ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu. Sikilizeni, kwa maana nina mambo muhimu ya kusema; ninafungua midomo yangu kusema lililo sawa. Kinywa changu husema lililo kweli, kwa maana midomo yangu huchukia uovu. Maneno yote ya kinywa changu ni haki; hakuna mojawapo lililopotoka wala ukaidi. Kwa wenye kupambanua yote ni sahihi; hayana kasoro kwa wale wenye maarifa. Chagua mafundisho yangu badala ya fedha, maarifa badala ya dhahabu safi, kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye. “Mimi hekima, nakaa pamoja na busara; ninamiliki maarifa na busara. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; ninachukia kiburi na majivuno, tabia mbaya na mazungumzo potovu. Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu; nina ufahamu na nina nguvu. Kwa msaada wangu wafalme hutawala na watawala hutunga sheria zilizo za haki, kwa msaada wangu wakuu hutawala, na wenye vyeo wote watawalao dunia. Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima viko kwangu, utajiri udumuo na mafanikio. Tunda langu ni bora kuliko dhahabu safi; kile nitoacho hupita fedha iliyo bora. Natembea katika njia ya unyofu katika mapito ya haki, nawapa utajiri wale wanipendao na kuzijaza hazina zao.

Shirikisha
Soma Methali 8