Methali 9:1-6
Methali 9:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hekima ameijenga nyumba yake, Amezichonga nguzo zake saba; Amechinja nyama zake, amechanganya divai yake, Ameiandalia meza yake pia. Amewatuma wajakazi wake, analia, Mahali pa mjini palipoinuka sana, Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, Njoo ule mkate wangu, Ukanywe divai niliyoichanganya. Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu.
Methali 9:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Hekima amejenga nyumba yake, nyumba yenye nguzo saba. Amechinja wanyama wa karamu, divai yake ameitayarisha, ametandika meza yake. Amewatuma watumishi wake wa kike mjini, waite watu kutoka kwenye vilele vya miinuko: “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!” Na yeyote aliye mpumbavu humwambia: “Njoo ukale chakula, na unywe divai niliyotengeneza. Achana na ujinga upate kuishi; fuata njia ya akili.”
Methali 9:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hekima umeijenga nyumba yake, Amezichonga nguzo zake saba; Amechinja nyama zake, umechanganya divai yake, Ameiandalia meza yake pia. Amewatuma wajakazi wake, analia, Mahali pa mjini palipoinuka sana, Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, Njoo ule mkate wangu, Ukanywe divai niliyoichanganya. Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu.
Methali 9:1-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo zake saba. Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake; pia ameandaa meza yake. Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita kutoka mahali pa juu sana pa mji. Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa! Njooni, mle chakula changu na mnywe divai niliyoichanganya. Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.