Zaburi 103:2-5
Zaburi 103:2-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai
Zaburi 103:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu! Usisahau kamwe wema wake wote. Ndiye anayenisamehe uovu wangu wote, na kuniponya magonjwa yote. Ndiye aniokoaye kutoka kifoni, na kunijalia rehema na fadhili zake. Ndiye anayeniridhisha mema maisha yangu yote, hata nabaki kijana mwenye nguvu kama tai.
Zaburi 103:2-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako kutoka kwa kaburi, Akutia taji la fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai
Zaburi 103:2-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usisahau wema wake wote, akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akuvika taji ya upendo na huruma, atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.