Nembo ya Programu ya Biblia
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 104:13-15 - Linganisha Matoleo Yote

Zaburi 104:13-15 BHN (Biblia Habari Njema)

Toka juu angani wainyeshea milima mvua, nayo dunia waitosheleza kwa baraka yako. Waotesha nyasi kwa ajili ya mifugo, na mimea kwa matumizi ya binadamu ili naye ajipatie chakula chake ardhini: Divai ya kumchangamsha, mafuta ya zeituni ya kumfurahisha, na mkate wa kumpa nguvu.

Shirikisha
Zaburi 104 BHN

Zaburi 104:13-15 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Huinywesha milima toka orofa zake; Nchi imeshiba mazao ya kazi zako. Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi, Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung’aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake.

Shirikisha
Zaburi 104 SUV

Zaburi 104:13-15 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Huinywesha milima toka juu angani; Nchi umeitosheleza kwa mazao ya kazi zako. Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi, Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung'aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake.

Shirikisha
Zaburi 104 SRUV

Zaburi 104:13-15 NEN (Neno)

Huinyeshea milima kutoka orofa zake, dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake. Huyafanya majani ya mifugo yaote, na mimea kwa watu kulima, wajipatie chakula kutoka ardhini: divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake, na mkate wa kutia mwili nguvu.

Shirikisha
Zaburi 104 NEN