Zaburi 119:56-62
Zaburi 119:56-62 Biblia Habari Njema (BHN)
Hii ni baraka kubwa kwangu, kwamba nazishika kanuni zako. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe riziki yangu kuu; naahidi kushika maneno yako. Naomba radhi yako kwa moyo wangu wote; unionee huruma kama ulivyoahidi! Nimeufikiria mwenendo wangu, na nimerudi nifuate maamuzi yako. Bila kukawia nafanya haraka kuzishika amri zako. Waovu wametega mitego waninase, lakini mimi sisahau sheria yako. Usiku wa manane naamka kukusifu, kwa sababu ya maagizo yako maadilifu.
Zaburi 119:56-62 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hayo ndiyo niliyokuwa nayo, Kwa sababu nimeyashika mausia yako. BWANA ndiye aliye fungu langu, Ninaahidi kuyatii maneno yake. Nimekuomba radhi kwa moyo wangu wote, Unifadhili kulingana na ahadi yako. Ninapozitafakari njia zako, Naielekeza miguu yangu kwa shuhuda zako. Nilifanya haraka wala sikukawia, Kuyatii maagizo yako. Japo kamba za wasio haki zimenifunga, Siisahau sheria yako. Usiku wa manane nitaamka nikushukuru, Kwa sababu ya hukumu zako za haki.
Zaburi 119:56-62 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hayo ndiyo niliyokuwa nayo, Kwa sababu nimeyashika mausia yako. BWANA ndiye aliye fungu langu, Nimesema kwamba nitayatii maneno yake. Nimekuomba radhi kwa moyo wangu wote, Unifadhili sawasawa na ahadi yako. Nalizitafakari njia zangu, Na miguu yangu nalizielekezea shuhuda zako. Nalifanya haraka wala sikukawia, Kuyatii maagizo yako. Kamba za wasio haki zimenifunga, Sikuisahau sheria yako. Katikati ya usiku nitaamka nikushukuru, Kwa sababu ya hukumu zako za haki.
Zaburi 119:56-62 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako. BWANA Ee BWANA, wewe ni fungu langu, nimeahidi kuyatii maneno yako. Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, nihurumie sawasawa na ahadi yako. Nimezifikiri njia zangu na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako. Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako. Hata waovu wanifunge kwa kamba, sitasahau sheria yako. Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki.