Zaburi 137:1-4
Zaburi 137:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Kando ya mito ya Babuloni, tulikaa, tukawa tunalia tulipokumbuka Siyoni. Katika miti ya nchi ile, tulitundika zeze zetu. Waliotuteka walitutaka tuwaimbie; watesi wetu walitutaka tuwafurahishe: “Tuimbieni mojawapo ya nyimbo za Siyoni!” Twawezaje kuimba wimbo wa Mwenyezi-Mungu katika nchi ya kigeni?
Zaburi 137:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni. Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu. Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka tuwatumbuize; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Twawezaje kuimba wimbo wa BWANA Katika nchi ya ugeni?
Zaburi 137:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni. Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu. Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Tuuimbeje wimbo wa BWANA Katika nchi ya ugeni?
Zaburi 137:1-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza tulipokumbuka Sayuni. Kwenye miti ya huko tulitundika vinubi vyetu, kwa maana huko hao waliotuteka walitaka tuwaimbie nyimbo, watesi wetu walidai nyimbo za furaha; walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!” Tutaimbaje nyimbo za BWANA, tukiwa nchi ya kigeni?