Zaburi 14:1-7
Zaburi 14:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema! Mwenyezi-Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni, aone kama kuna yeyote mwenye busara, kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu. Lakini wote wamekosa, wote wamepotoka pamoja; hakuna atendaye mema, hakuna hata mmoja. “Je, hao watendao maovu hawana akili? Wanawatafuna watu wangu kama mikate; wala hawanijali mimi Mwenyezi-Mungu.” Hapo watashikwa na hofu kubwa, maana Mungu yu pamoja na waadilifu. Unaweza kuvuruga mipango ya maskini, lakini Mwenyezi-Mungu ndiye kimbilio lake. Laiti ukombozi wa Israeli ungefika kutoka Siyoni! Mwenyezi-Mungu atakaporekebisha hali ya watu wake, wazawa wa Yakobo watashangilia; Waisraeli watafurahi.
Zaburi 14:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja. Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti BWANA. Hapo ndipo waovu watakaposhikwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki. Mnaiharibu mipango ya mtu mnyonge, Bali BWANA ndiye aliye kimbilio lake. Laiti wokovu wa Israeli ungetoka katika Sayuni! BWANA awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.
Zaburi 14:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja. Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti BWANA. Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki. Mnalitia aibu shauri la mtu mnyonge, Bali BWANA ndiye aliye kimbilio lake. Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! BWANA awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.
Zaburi 14:1-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna hata mmoja atendaye mema. BWANA anawachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wowote wanaomtafuta Mungu. Wote wamepotoka, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja! Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza: wale ambao huwala watu wangu kama watu walavyo mkate, hao ambao hawamwiti BWANA? Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu, maana Mungu yupo pamoja na wenye haki. Ninyi watenda mabaya mnakwamisha mipango ya maskini, bali BWANA ndiye kimbilio lao. Laiti wokovu wa Israeli ungalikuja kutoka Sayuni! Wakati BWANA arejeshapo wafungwa wa watu wake, Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi!