Nembo ya Programu ya Biblia
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 15:1-3 - Linganisha Matoleo Yote

Zaburi 15:1-3 BHN (Biblia Habari Njema)

Nani ee Mwenyezi-Mungu atakayekaa hemani mwako? Nani atakayeishi juu ya mlima wako mtakatifu? Ni mtu aishiye bila lawama, atendaye daima yaliyo mema, asemaye ukweli kutoka moyoni; ni mtu asiyesengenya watu, asiyemtendea uovu rafiki yake, wala kumfitini jirani yake

Shirikisha
Zaburi 15 BHN

Zaburi 15:1-3 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu? Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake.

Shirikisha
Zaburi 15 SUV

Zaburi 15:1-3 SRUV (Swahili Revised Union Version)

BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayeishi Katika kilima chako kitakatifu? Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala kumtenda mwenziwe mabaya, Wala kumsengenya jirani yake.

Shirikisha
Zaburi 15 SRUV

Zaburi 15:1-3 NEN (Neno)

BWANA, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu? Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake, na hana masingizio ulimini mwake, asiyemtenda jirani yake vibaya, na asiyemsingizia mwenzake

Shirikisha
Zaburi 15 NEN