Zaburi 150:1-6
Zaburi 150:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Msifuni Mungu katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu zake kuu. Msifuni kwa sababu ya matendo yake makuu; msifuni kwa ajili ya utukufu wake mkuu. Msifuni kwa mlio wa tarumbeta; msifuni kwa zeze na kinubi! Msifuni kwa ngoma na kucheza; msifuni kwa filimbi na banjo! Msifuni kwa kupiga matoazi. Msifuni kwa matoazi ya sauti kubwa. Kila kiumbe hai kimsifu Mwenyezi-Mungu! Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Zaburi 150:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.
Zaburi 150:1-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Msifuni BWANA. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu. Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze, msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi, msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila chenye pumzi na kimsifu BWANA.
Zaburi 150:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)