Zaburi 30:2-5
Zaburi 30:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, nilikulilia msaada, nawe ukaniponya. Ee Mwenyezi-Mungu, umeniokoa kutoka kuzimu; umenipa tena uhai, umenitoa miongoni mwa waendao kuzimu. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu sifa, enyi waaminifu wake; kumbukeni utakatifu wake na kumshukuru. Hasira yake hudumu kitambo kidogo, wema wake hudumu milele. Kilio chaweza kuwapo hata usiku, lakini asubuhi huja furaha.
Zaburi 30:2-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, Mungu wangu, Nilikulilia ukaniponya. Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao Shimoni. Mwimbieni BWANA zaburi, Enyi watauwa wake. Na kutoa shukrani. Kwa kukumbuka utakatifu wake. Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu; Radhi yake ni ya milele. Kilio huweza kuwapo usiku, Lakini furaha huja asubuhi.
Zaburi 30:2-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya. Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni. Mwimbieni BWANA zaburi, Enyi watauwa wake. Na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake. Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.
Zaburi 30:2-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya. Ee BWANA, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. Mwimbieni BWANA, enyi watakatifu wake; lisifuni jina lake takatifu. Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha.