Zaburi 5:1-3
Zaburi 5:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Usikilize maneno yangu, ee Mwenyezi-Mungu, usikie ninavyopiga kite. Usikilize kilio changu, Mfalme wangu na Mungu wangu, maana wewe ndiwe nikuombaye. Ee Mwenyezi-Mungu, alfajiri waisikia sauti yangu, asubuhi nakutolea tambiko yangu, kisha nangojea unijibu.
Zaburi 5:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, uyasikilize maneno yangu, Ukuangalie kutafakari kwangu. Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye. BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.
Zaburi 5:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, uyasikilize maneno yangu, Ukuangalie kutafakari kwangu. Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye. BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.
Zaburi 5:1-3 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee Mwenyezi Mungu, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu. Sikiliza kilio changu ili unisaidie, Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana kwako ninaomba. Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Mwenyezi Mungu; asubuhi naleta haja zangu mbele zako, na kusubiri kwa matumaini.