Zaburi 72:12-19
Zaburi 72:12-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi. Atawahurumia wanyonge na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa. Atawakomboa kutoka kwa maonevu na udhalimu, Maana damu yao ina thamani machoni pake. Na aishi maisha marefu! Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa. Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawayewaye kama ilivyo katika milima ya Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi. Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua, umaarufu wake uwepo; Mataifa yote na wabarikiwe katika yeye, Na kumwita heri. Na ahimidiwe BWANA, Mungu, Mungu wa Israeli, Atendaye miujiza Yeye peke yake; Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.
Zaburi 72:12-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi. Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa. Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu, Na damu yao ina thamani machoni pake. Basi na aishi; Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa. Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawaye-waye kama Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi. Jina lake na lidumu milele, Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao; Mataifa yote na wajibariki katika yeye, Na kumwita heri. Na ahimidiwe BWANA, Mungu, Mungu wa Israeli, Atendaye miujiza Yeye peke yake; Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.
Zaburi 72:12-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Anamkomboa fukara anayemwomba, na maskini asiye na wa kumsaidia. Anawahurumia watu dhaifu na fukara, anayaokoa maisha yao wenye shida. Anawatoa katika udhalimu na ukatili, maana maisha yao ni ya thamani kubwa kwake. Mfalme na aishi maisha marefu; apokee zawadi ya dhahabu kutoka Sheba; watu wamwombee kwa Mungu daima, na kumtakia baraka mchana kutwa. Nchi na izae nafaka kwa wingi, vilima vijae mavuno kama ya Lebanoni, na watu mijini wastawi kama nyasi. Jina la mfalme litukuke daima; fahari yake idumu pindi liangazapo jua. Kwake mataifa yote yabarikiwe; watu wote wamwite mbarikiwa! Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye peke yake hufanya miujiza. Jina lake tukufu na litukuzwe milele; utukufu wake ujae ulimwenguni kote! Amina, Amina!
Zaburi 72:12-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, aliyeonewa asiye na wa kumsaidia. Atawahurumia wanyonge na wahitaji na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti. Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, kwani damu yao ni ya thamani machoni pake. Aishi maisha marefu! Na apewe dhahabu ya Sheba. Watu wamwombee daima na kumbariki mchana kutwa. Nafaka ijae tele katika nchi yote, juu ya vilele vya vilima na istawi. Tunda lake na listawi kama Lebanoni, listawi kama majani ya kondeni. Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, nao watamwita aliyebarikiwa. BWANA Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa, yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu. Jina lake tukufu lisifiwe milele, ulimwengu wote ujae utukufu wake. Amen na Amen.