Zaburi 78:1-8
Zaburi 78:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Sikieni mafundisho yangu, enyi watu wangu; yategeeni sikio maneno ya kinywa changu. Nitasema nanyi kwa mafumbo, nitasema mambo yaliyofichika tangu kale; mambo tuliyoyasikia na kuyajua, mambo ambayo wazee wetu walitusimulia. Hatutawaficha watoto wetu; ila tutakisimulia kizazi kijacho matendo matukufu ya Mwenyezi-Mungu na uwezo wake; tutawaambia maajabu yake aliyotenda. Aliwapa wazawa wa Yakobo masharti, aliweka sheria katika Israeli, ambayo aliwaamuru wazee wetu wawafundishe watoto wao; ili watu wa kizazi kijacho, watoto watakaozaliwa baadaye, wazijue, nao pia wawajulishe watoto wao, ili wamwekee Mungu tumaini lao, wasije wakasahau matendo ya Mungu, bali wazingatie amri zake. Wasiwe kama walivyokuwa wazee wao, watu wakaidi na waasi; kizazi ambacho hakikuwa na msimamo thabiti, ambacho hakikuwa na uaminifu kwa Mungu.
Zaburi 78:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu, Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu. Nitafumbua kinywa changu kwa mithali, Niyatamke mafumbo ya kale. Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu, Ambayo baba zetu walituambia. Hayo hatutawaficha wana wao, Huku tukiwaambia kizazi kingine, Sifa za BWANA, na nguvu zake, Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya. Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, Na sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu Wawajulishe wana wao, Ili kizazi kingine wawe na habari, Ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao. Wamwekee Mungu tumaini lao. Wala wasiyasahau matendo ya Mungu, Bali wazishike amri zake. Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.
Zaburi 78:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu, Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu. Na nifunue kinywa changu kwa mithali, Niyatamke mafumbo ya kale. Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu, Ambayo baba zetu walituambia. Hayo hatutawaficha wana wao, Huku tukiwaambia kizazi kingine, Sifa za BWANA, na nguvu zake, Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya. Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, Na sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu Wawajulishe wana wao, Ili kizazi kingine wawe na habari, Ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao Wamwekee Mungu tumaini lao. Wala wasiyasahau matendo ya Mungu, Bali wazishike amri zake. Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.
Zaburi 78:1-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu, sikilizeni maneno ya kinywa changu. Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo, nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale: yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia. Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya BWANA, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya. Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao, ili kizazi kijacho kizijue, pamoja na watoto ambao watazaliwa, nao pia wapate kuwaeleza watoto wao. Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, nao wasingesahau matendo yake, bali wangalizishika amri zake. Ili wasifanane na baba zao, waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi, ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwake, ambao roho zao hazikumwamini.