Zaburi 94:17-19
Zaburi 94:17-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu, Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya. Niliposema, Mguu wangu unateleza; Ee BWANA, fadhili zako zilinitegemeza. Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu, Faraja zako zaifurahisha roho yangu.
Zaburi 94:17-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asingalinisaidia, ningalikwisha kwenda kwenye nchi ya wafu. Nilipohisi kwamba ninateleza, fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, zilinitegemeza. Mahangaiko ya moyo wangu yanapozidi, wewe wanifariji na kunifurahisha.
Zaburi 94:17-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu, Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya. Niliposema, Mguu wangu unateleza; Ee BWANA, fadhili zako zilinitegemeza. Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu, Faraja zako zinaifurahisha roho yangu.
Zaburi 94:17-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kama BWANA asingelinisaidia upesi, ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo. Niliposema, “Mguu wangu unateleza,” Ee BWANA, upendo wako ulinishikilia. Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu, faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu.