Ufunuo 12:14-16
Ufunuo 12:14-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hadi mahali pake, hapo alishwapo kwa nyakati tatu na nusu, mbali na nyoka huyo. Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, ili achukuliwe na mto ule. Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule lililoutoa lile joka katika kinywa chake.
Ufunuo 12:14-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini mama huyo akapewa mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sana na hilo joka, mpaka mahali pake jangwani ambapo angehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Basi, joka likatapika maji mengi kama mto, yakamfuata huyo mama nyuma ili yamchukue. Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: Ikajifunua kama mdomo na kuyameza maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka.
Ufunuo 12:14-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
Ufunuo 12:14-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini huyo mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai mkubwa, kusudi aweze kuruka mpaka mahali palipotayarishwa kwa ajili yake huko jangwani, ambako atatunzwa kwa wakati na nyakati na nusu, ya wakati ambako yule joka hawezi kufika. Ndipo lile joka likamwaga maji kama mto kutoka kinywani mwake, ili kumfikia huyo mwanamke na kumkumba kama mafuriko. Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao huyo joka alikuwa ameutoa kinywani mwake.