Ufunuo 9:3-4
Ufunuo 9:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi. Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu chochote kilicho kibichi, wala mti wowote, ila wale watu wasio na mhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao.
Ufunuo 9:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo katika ule moshi wakatoka nzige wakaenda juu ya nchi, nao wakapewa nguvu kama zile za nge wa duniani. Wakaambiwa wasidhuru nyasi ya nchi, wala mmea wala mti wowote, bali wawadhuru tu wale watu ambao hawana muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao.
Ufunuo 9:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Nzige wakatoka katika moshi huo, wakaingia duniani, wakapewa nguvu kama ya nge. Wakaamrishwa wasiharibu nyasi za nchi wala majani wala miti yoyote, bali wawaharibu wale tu ambao hawakupigwa mhuri wa Mungu katika paji la uso.
Ufunuo 9:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi. Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.