Wimbo Ulio Bora 7:1-4
Wimbo Ulio Bora 7:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyayo zako katika viatu zapendeza sana! Ewe mwanamwali wa kifalme. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, kazi ya msanii hodari. Kitovu chako ni kama bakuli lisilokosa divai iliyokolezwa. Tumbo lako ni kama lundo la ngano lililozungushiwa yungiyungi kandokando. Matiti yako ni kama paa mapacha, ni kama swala wawili. Shingo yako ni kama mnara wa pembe za ndovu; macho yako ni kama vidimbwi mjini Heshboni, karibu na mlango wa Beth-rabi. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, ambao unauelekea mji wa Damasko.
Wimbo Ulio Bora 7:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Binti wa kimalkia, jinsi ulivyo mzuri Hatua zako katika mitarawanda. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, Kazi ya mikono ya fundi stadi; Kitovu chako ni kama bakuli la mviringo, Na isikose divai iliyochanganyika; Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano, Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro; Matiti yako mawili ni kama wanapaa wawili, Ambao ni mapacha ya paa; Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe; Macho yako kama viziwa vya Heshboni, Karibu na mlango wa Beth-rabi; Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, Unaoelekea Dameski
Wimbo Ulio Bora 7:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Siti msharifu, jinsi zilivyo nzuri Hatua zako katika mitalawanda. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, Kazi ya mikono ya fundi mstadi; Kitovu chako ni kama bilauri iliyoviringana, Na isikose divai iliyochanganyika; Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano, Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro; Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili, Ambao ni mapacha ya paa; Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe; Macho yako kama viziwa vya Heshboni, Karibu na mlango wa Beth-rabi; Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, Unaoelekea Dameski
Wimbo Ulio Bora 7:1-4 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee binti ya mwana wa mfalme, tazama jinsi inavyopendeza miguu yako katika viatu! Miguu yako yenye madaha ni kama vito vya thamani, kazi ya mikono ya fundi stadi. Kitovu chako ni kama bilauri ya mviringo ambayo kamwe haikosi divai iliyochanganywa. Kiuno chako ni kichuguu cha ngano kilichozungukwa kwa yungiyungi. Matiti yako ni kama wana-paa wawili, mapacha wa paa. Shingo yako ni kama mnara wa pembe ya ndovu. Macho yako ni vidimbwi vya Heshboni karibu na lango la Beth-Rabi. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni ukitazama kuelekea Dameski.