Zekaria 8:16-17
Zekaria 8:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Hivi ndivyo mnavyopaswa kufanya: Kila mmoja wenu na amwambie mwenzake ukweli. Mahakama yenu daima na yatoe hukumu za haki ziletazo amani. Mtu yeyote miongoni mwenu asikusudie kutenda uovu dhidi ya mwenzake, wala msiape uongo, maana nayachukia sana matendo hayo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Zekaria 8:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme ukweli na jirani yake; katika malango yenu toeni hukumu za kweli na ziletazo amani; wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA.
Zekaria 8:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme kweli na jirani yake; hukumuni kweli na hukumu ya amani malangoni mwenu; wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA.