Zekaria 9:1-8
Zekaria 9:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ufunuo wa neno la BWANA, lililosemwa juu ya nchi ya Hadraki, na Dameski itakuwa mahali pake pa kustarehe; kwa maana jicho la mwanadamu na la kabila zote za Israeli linamwelekea BWANA; na Hamathi pia iliyo mpakani mwake; na Tiro, na Sidoni, kwa maana ana akili nyingi. Na Tiro alijijengea ngome, akakusanya fedha kama mchanga, dhahabu safi kama matope ya njia kuu. Tazama, Bwana atamwondolea mali zake, naye ataupiga uwezo wake alio nao baharini, naye mwenyewe atateketezwa kwa moto. Ashkeloni ataona haya na kuogopa; Gaza pia, naye atafadhaika sana; na Ekroni, kwa maana matarajio yake yatatahayarika; na mfalme ataangamia toka Gaza, na Ashkeloni atakuwa hana watu. Na mwana wa haramu atatawala huko Ashdodi, nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. Nami nitaondoa damu yake kinywani mwake, na machukizo yake nitayatoa katika meno yake; yeye naye atakuwa ni mabaki kwa Mungu wetu; naye atakuwa kama mtu mkuu katika Yuda, na Ekroni kama Myebusi. Nami nitapiga kambi yangu pande zote za nyumba yangu ili kuwapinga adui, mtu awaye yote asipite ndani yake wala kurudi; wala mtu aoneaye hatapita tena kati yao; kwa maana sasa nimeona kwa macho yangu.
Zekaria 9:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ufunuo wa neno la BWANA, lililosemwa juu ya nchi ya Hadraki, na Dameski itakuwa mahali pake pa kustarehe; kwa maana jicho la mwanadamu na la kabila zote za Israeli linamwelekea BWANA; na Hamathi pia iliyo mpakani mwake; na Tiro, na Sidoni, kwa maana ana akili nyingi. Na Tiro alijijengea ngome, akakusanya fedha kama mchanga, dhahabu safi kama matope ya njia kuu. Tazama, Bwana atamwondolea mali zake, naye ataupiga uwezo wake alio nao baharini, naye mwenyewe atateketezwa kwa moto. Ashkeloni ataona haya na kuogopa; Gaza pia, naye atafadhaika sana; na Ekroni, kwa maana taraja lake litatahayarika; na mfalme ataangamia toka Gaza, na Ashkeloni atakuwa hana watu. Na mwana wa haramu atatawala huko Ashdodi, nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. Nami nitaondoa damu yake kinywani mwake, na machukizo yake nitayatoa katika meno yake; yeye naye atakuwa ni mabaki kwa Mungu wetu; naye atakuwa kama mtu mkuu katika Yuda, na Ekroni kama Myebusi. Nami nitapiga kambi yangu pande zote za nyumba yangu ili kuwapinga adui, mtu awaye yote asipite ndani yake wala kurudi; wala mtu aoneaye hatapita tena kati yao; kwa maana sasa nimeona kwa macho yangu.
Zekaria 9:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Kauli ya Mwenyezi-Mungu: Mwenyezi-Mungu ametamka siyo tu dhidi ya nchi ya Hadraki bali pia dhidi ya Damasko. Maana nchi ya Aramu ni mali ya Mwenyezi-Mungu, kama vile yalivyo makabila yote ya Israeli. Hali kadhalika mji wa Hamathi unaopakana na Hadraki; na hata miji ya Tiro na Sidoni ingawaje yajiona kuwa na hekima sana. Mji wa Tiro umejijengea ngome kumbwa, umejirundikia fedha kama vumbi, na dhahabu kama takataka barabarani. Lakini Bwana ataichukua mali yake yote, utajiri wake atautumbukiza baharini, na kuuteketeza mji huo kwa moto. Mji wa Ashkeloni utaona hayo na kuogopa, nao mji wa Gaza utagaagaa kwa uchungu; hata Ekroni, maana tumaini lake litatoweka. Mji wa Gaza utapoteza mfalme wake, nao Ashkeloni hautakaliwa na watu. Mji wa Ashdodi utakaliwa na machotara. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kiburi cha Filistia nitakikomesha. Nitawakomesha kula nyama yenye damu, na chakula ambacho ni chukizo. Mabaki watakuwa mali yangu, kama ukoo mmoja katika Yuda. Watu wa Ekroni watakuwa kama Wayebusi. Mimi mwenyewe nitailinda nchi yangu, nitazuia majeshi yasipitepite humo. Hakuna mtu atakayewadhulumu tena watu wangu, maana, kwa macho yangu mwenyewe, nimeona jinsi walivyoteseka.”
Zekaria 9:1-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Neno: Neno la BWANA liko kinyume na nchi ya Hadraki na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika, kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote za Israeli yako kwa BWANA, pia juu ya Hamathi inayopakana nayo, juu ya Tiro na Sidoni, ingawa wana ujuzi mwingi sana. Tiro amejijengea ngome imara, amelundika fedha kama mavumbi na dhahabu kama taka za mitaani. Lakini Bwana atamwondolea mali zake na kuuangamiza uwezo wake wa baharini, naye atateketezwa kwa moto. Ashkeloni ataona hili na kuogopa; Gaza atagaagaa kwa maumivu makali, pia Ekroni, kwa sababu matumaini yake yatanyauka. Gaza atampoteza mfalme wake na Ashkeloni ataachwa pweke. Wageni watakalia mji wa Ashdodi, nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. Nitaondoa damu vinywani mwao, chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao. Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu, nao watakuwa viongozi katika Yuda, naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi. Lakini nitailinda nyumba yangu dhidi ya majeshi ya wanyangʼanyi. Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena, kwa maana sasa ninawachunga.