Uwekezaji Wako Ulio Bora!Mfano
“Soma Biblia Mara kwa Mara”
Wengi wetu tutakubali kwamba Biblia imejaa mambo mengi ya kusoma – baadhi yake yakionekana kutuzidi na hayaeleweki wakati mwingine. Hapa ni kweli chache juu ya Biblia ambazo zitakusaidia unaposoma kuweza kufanya rejea na kuelewa vizuri.
Kwanza, utagundua kwamba Biblia imegawanyika katika sehemu mbili:
Agano la Kale ni mkusanyiko wa maandiko yanayoanzia na uumbaji wa ulimwengu, historia ya watu wa Israeli – pamoja na kushindwa kwao kama taifa, kuchukuliwa kwao mateka na maadui zao, na mwishoni kurudi kwao tena na kuimiliki Yerusalemu mamia ya miaka michache kabla ya kuzaliwa kwa Kristo. Agano la Kale pia ni sheria ya Mungu kwa Waisraeli.
Agano Jipya ni mkusanyiko wa maandiko kuanzia muda kidogo tu kabla kuzaliwa kwa Yesu, maisha na huduma Yake, kifo Chake na kufufuka Kwake kama mwokozi, na pia kuanzishwa na kupanuka kwa kanisa lake ulimwenguni pote. Ujumbe wa uhuru katika Kristo kwa neema kama unavyofunuliwa katika Agano Jipya unatimiza na kufanyika mbadala wa taratibu zilizowekwa katika Agano la Kale.
Pili, na kwa kawaida, kuna aina tatu za maandiko utakayoyaona katika Agano la Kale na Agano Jipya katika Biblia:
Matukio ya Kihistoria - maandiko yanayoelezea simulizi za kweli na kutoa historia ya watu na matukio muhimu.
Maandiko yenye Maelekezo – vitabu na aya zinazotoa maelekezo juu ya mambo mengi ya maisha ya Kikristo, utaratibu wa kanisa mambo binafsi na mambo ya kifamilia bila kutoa mlolongo wa historia ya matukio.
Maandiko yenye kuvutia -mashairi, maandiko ya kisanii yenye lengo la kutia moyo, kuinua na kuonyesha hisia toka kwa mwandishi kwenda kwa msomaji.
Maandiko ya Agano Jipya yanayotoa Matukio ya Kihistoria ya maisha na huduma ya Yesu Kristo ni Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Vitabu hivi vine pia vinaitwa Injili. Kitabu cha Matendo ya Mitume ni kitabu kingine cha historia katika Agano Jipya ambacho kinabainisha kuanzishwa na kupanuka kwa kanisa baada ya kifo cha Yesu na kufufuka kwake.
Vitabu vya Agano Jipya vinavyohusisha Maandiko ya Maelekezo ni Warumi mpaka Yuda. Hizi barua halisi kutoka viongozi wa kanisa zikitoa ushauri na maelekezo kwa Wakristo wengine na makanisa ulimwenguni pote.
Kitabu cha Agano la Kale cha Zaburi ni mfano bora wa maandiko yenye kuvutia. Hapa chini ni maandiko yenye kuvutia kutoka Zaburi yanayotuhakikishia baraka ambazo Mungu humpatia mtu ambaye huwekeza Neno la Mungu mara kwa mara katika maisha yake.
“Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.” Zaburi 1:2-3
Kupanda mbegu ya Neno la Mungu katika maisha yetu, tunahitaji kufanya usomaji wa Biblia sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Pale mbegu ya Neno la Mungu inaposhamiri katika maisha yako, baraka zake zitadhihirika zaidi. Utapokea nguvu kutoka Neno Lake kukusaidia, hata katika wakati wa ukame na magumu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kupata matunda tele na ya baraka huanzia na kufanya uwekezaji ulio sahihi. Kama wewe ni mkristo mpya, hakuna uwekezaji ulio mkuu zaidi unaoweza kufanya katika imani yako zaidi ya kuingiza ndani yako Neno la Mungu mara kwa mara. Anzia hapa ikusaidie Kusoma, Kuelewa na Kutumia kwa ufanisi kila siku. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)