Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Tohara ya Kristo ni kuondolewa dhambi moyoni. Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo (m.11). Hufanyika katika ubatizo. Mtu akitahiriwa ni tendo analofanyiwa na wengine. Vilevile na ubatizo wetu. Kuokoka kwetu ni tendo la Mungu peke yake. Yeye ndiye anayetuunganisha na kufa na kufufuka kwake Yesu kwa ajili yetu. Mkazikwa pamoja naye [Yesu] katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu (m.12). Hapo ndipo anapotuingiza kwa imani katika ufalme wake. Anafanya agano nasi kama alivyowaingiza Wayahudi katika agano la Sinai walipotahiriwa. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa (Mk 16:16).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/