Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

SIKU 3 YA 30

Mara kwa mara Yesu alitumia muda kwa ajili ya sala, ila mara nyingi haikuandikwa aliomba nini. Katika sura hii ya 17 tumepewa mfano mmoja wa sala aliyoiomba Yesu. 1. Sala inamhusu yeye mwenyewe na uhusiano wake na Baba. Kusudi kubwa la kazi ya Yesu ni kumtukuza Baba yake (m.1, Akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe). 2. Sala inawahusu waliompokea na kumwamini Yesu (m.2-3, Ulimpa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma). Kama wewe ni mmoja wao umepewa baraka ya pekee ya kuombewa na Yesu kwa Mungu! Yesu anasema: "Siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa" (m.9).

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana