Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Leo tumepewa mfano mzuri jinsi ya kuifanya kazi ya Bwana ikiingia katika mapambano makali na kupata vitisho kutoka kwa watu:1.Tuwaendee waumini wenzetu na kuwashirikisha matatizo yetu, kama walivyofanya Wakristo wa kwanza:Walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee(m.23).2.Tufanye mkutano wa kuomba wote pamoja ili kumlilia Bwana atusaidie:Wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo(m.24)!Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wakokunenaneno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu(m.29-30).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/