Mwanzo 14
14
Abramu anamwokoa Loti
1Wakati huo, mfalme Amrafeli wa Shinari, mfalme Arioko wa Elasari, mfalme Kedorlaomeri wa Elamu na mfalme Tidali wa Goiimu, 2walipigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, dhidi ya Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na dhidi ya mfalme wa Bela (yaani Soari). 3Wafalme hao watano waliyaunganisha majeshi yao katika bonde la Sidimu (yaani Bahari ya Chumvi).#14:3 Bahari ya Chumvi: Inaitwa pia “Bahari ya Araba” (Kumb 3:17). 4Kwa muda wa miaka kumi na miwili walikuwa wakimtii mfalme Kedorlaomeri, lakini mnamo mwaka wa kumi na tatu, walimwasi. 5Mnamo mwaka wa kumi na nne, mfalme Kedorlaomeri na wale wafalme wenzake walikuja na kuwashinda watu wa Refaimu#14:5 Watu wa Refaimu: Warefaimu, Wazuzi na Waemi walikuwa wakazi wa kale wa eneo lililoko mashariki ya mto Yordani. Taz Kumb 2:10-11 maelezo. huko Ashtaroth-karnaimu, na Wazuzi huko Hamu, na Waemi huko Shawe-kiriathaimu, 6na Wahori huko mlimani kwao Seiri, wakawafukuza hadi Elparani, mpakani mwa jangwa. 7Kisha wakarudi nyuma mpaka Enmishpati#14:7 Enmishpati: Katika Kiebrania jina hili lina maana ya “Kisima cha Hukumu” na ni jina lingine la “Kadeshi” au “Kadesh-barnea”, chemchemi ya jangwani kusini mwa Beersheba katika jangwa la Negebu (taz Mwa 12:9 maelezo). (yaani Kadeshi), wakaivamia nchi yote ya Waamaleki,#14:7 Waamaleki: Kabila moja katika peninsula ya Sinai (taz Kut 17:8). Na, kuhusu “Waamori” taz Mwa 15:16. na kuwashinda Waamori waliokaa Hasason-tamari.
8Ndipo mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboimu na mfalme wa Bela 9(yaani Soari), wakaingia vitani katika bonde la Sidimu kupigana na Kedorlaomeri mfalme wa Elamu, Tidali mfalme wa Goiimu, Amrafeli mfalme wa Shinari na Arioko mfalme wa Elasari; wafalme wanne dhidi ya wafalme watano. 10Bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami; kwa hiyo wafalme wa Sodoma na Gomora walipokuwa wakiikimbia vita, wakatumbukia humo, lakini wengine wakatorokea mlimani. 11Basi, wale walioshinda, wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora, kadhalika na mazao yao, wakaenda zao. 12Walimteka hata Loti, mwana wa nduguye Abramu#14:12 Loti, mwana wa nduguye Abramu: Rejea Mwa 13:12; 19:1-29. aliyekuwa anakaa Sodoma, pamoja na mali yake, wakaenda zao.
13Mtu mmoja aliyeponyoka, akaenda kumwarifu yule Mwebrania Abramu#14:13 Mwebrania Abramu: Neno “Mwebrania” linatumika mara chache sana katika A.K. Majina yanayofanana na hili ni “apiru” au “habiru” na yalitumiwa mara nyingi katika Mashariki ya Kati ya Kale. Jina hilo lilitumiwa kutaja kikundi cha watu ambao hawakuingizwa katika jumuiya na kwa namna moja au nyingine lilitumika kwa dharau kiasi fulani. Taz Mwa 10:21 na 1Sam 14:11. ambaye alikuwa anaishi karibu na mialoni ya Mwamori#14:13 Mialoni ya Mamre, Mwamori: Taz Mwa 13:18. Mamre.#14:13 Mamre: Jina hili hapo awali lilitajwa kama jina la mahali lakini sasa linatumika kama jina la mtu. Na kuhusu “Mwamori” taz Mwa 15:16 maelezo. Mamre alikuwa ndugu yake Eshkoli#14:13 Eshkoli: Katika Hes 13:23-24 ni jina la bonde karibu na Hebroni. na Aneri. Wote walikuwa wamefanya agano na Abramu. 14Abramu alipopata habari kwamba mpwa wake amechukuliwa mateka, akatoka na watu wake stadi 318 waliozaliwa katika nyumba yake, akawafuatia adui mpaka Dani.#14:14 Dani: Jina hili hapa linataja kwa jumla sehemu ya kaskazini kabisa ya Palestina. Rejea Amu 20:1. 15Huko, akaligawa jeshi lake katika makundi. Usiku, akawashambulia adui zake, akawashinda na kuwafukuza hadi Hoba, kaskazini mwa Damasko. 16Basi, Abramu akaikomboa mali yote iliyotekwa na adui, na kumkomboa Loti mpwa wake, mali yake, pamoja na wanawake na watu wengine.
Melkisedeki anambariki Abramu
17Abramu aliporudi baada ya kumshinda mfalme Kedorlaomeri na wenzake, mfalme wa Sodoma alitoka kwenda kumlaki katika bonde la Shawe, (yaani Bonde la Mfalme).#14:17 Bonde la Mfalme: Yahusu, bila shaka, bonde moja karibu na mji wa Yerusalemu na ambalo linatajwa pia katika 2Sam 18:18. 18Naye Melkisedeki,#14:18 Melkisedeki: Jina hili hapo awali lilikuwa na maana ya “Sedeki ni mfalme”. Kama ilivyokuwa desturi nyakati za huko Mashariki ya Kati ya Kale mfalme alikuwa pia kasisi au kuhani. Katika A.J. jina hili “Melkisedeki” linafafanuliwa kwa maana ya “mfalme wa uadilifu” (rejea Ebr 7:2). mfalme wa mji wa Salemu,#14:18 Salemu: Yaani Yerusalemu (taz Zab 76:2 maelezo), mji uliotwaliwa na Daudi na baadaye ukawa mji mkuu wa utawala wake. ambaye alikuwa kuhani wa Mungu Mkuu, akaleta mkate na divai,#14:18 Mkate na divai: Katika A.J. Melkisedeki ameoneshwa kuwa mfano wa Kristo, yaani kuhani mkuu wa A.J. (rejea Ebr 5:6-10; 6:20; 7). 19akambariki Abramu akisema,
“Abramu na abarikiwe na Mungu Mkuu,#14:19 Mungu Mkuu: Kiebrania ni “El Elyon”. Yawezekana kwamba “El Elyon” alikuwa mungu mkuu wa wakazi wa Yerusalemu kabla ya Waisraeli kuweko hapo. Kisa hiki, kwa uchache, kinaonesha kwamba Melkisedeki, ambaye alikuwa mfalme na kuhani lakini hakuwa Mwebrania, pamoja na Abrahamu, babu wa Wayahudi, walimwabudu Mungu yule yule aliye Muumba wa ulimwengu, lakini kwa majina tofauti.
Muumba mbingu na dunia!
20Na atukuzwe Mungu Mkuu,
aliyewatia adui zako mikononi mwako!”
Naye Abramu akampa Melkisedeki mchango wake sehemu ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo.#14:20 Abramu akampa …sehemu ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo: Rejea Ebr 7:4-10. Kwa maeneo mengine, “sehemu ya kumi” ni “asilimia kumi”.
21Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu, lakini jichukulie mali yote wewe mwenyewe.” 22Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu, aliyeumba mbingu na dunia, 23kwamba sitachukua uzi au kamba ya kiatu, wala chochote kilicho chako, usije ukajivuna na kusema kwamba umenitajirisha. 24Basi, sitachukua chochote isipokuwa tu vile vitu vijana wangu walivyokula na sehemu ya wale waliokuwa pamoja nami, Aneri, Eshkoli na Mamre ambao wana haki nayo.”
ที่ได้เลือกล่าสุด:
Mwanzo 14: BHNTLK
เน้นข้อความ
แบ่งปัน
คัดลอก
ต้องการเน้นข้อความที่บันทึกไว้ตลอดทั้งอุปกรณ์ของคุณหรือไม่? ลงทะเบียน หรือลงชื่อเข้าใช้
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993

: