Mwanzo 8
8
Kupwa kwa gharika
1 #
Mwa 19:29; Kut 2:24; 1 Sam 1:19; Zab 105:42; 136:23; Kut 14:21; 15:10; Zab 104:7 Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua; 2#Mwa 7:11; 1 Fal 8:35; Ayu 38:37 chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa; 3#Mwa 7:24 maji yakadumu kuondoka katika nchi; na mwisho wa siku mia moja na hamsini maji yakapunguka. 4Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya milima ya Ararati. 5Maji yakapungukapunguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana. 6#Mwa 6:16 Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya; 7#1 Fal 17:4 akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huku na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi. 8Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi; 9#Kum 28:65 bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani.
10Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili, 11#Lk 2:14 njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelichuma, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi. 12Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe.
13Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka. 14Na mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa kavu.
15Mungu akamwambia Nuhu, akisema, 16#Mwa 7:13; Zab 121:8 Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe. 17#Mwa 1:22 Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi. 18Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; 19kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa aina zao, wakatoka katika safina.
Ahadi ya Mungu kwa Nuhu
20 #
Law 11:1-31
Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. 21#Law 1:9; Kut 29:41; 2 Kor 2:15; Efe 5:2; Mwa 3:17; 6:17; Isa 54:9; Mwa 6:5; Zab 51:5; Ayu 14:4; 15:14; Yer 17:9; Rum 1:21; 3:23; Efe 2:1-3; Mwa 9:15 BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. 1 22#Yer 33:20,25 Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa joto, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Kasalukuyang Napili:
Mwanzo 8: RSUVDC
Haylayt
Ibahagi
Kopyahin
Gusto mo bang ma-save ang iyong mga hinaylayt sa lahat ng iyong device? Mag-sign up o mag-sign in
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.