Mathayo 2:12-13

Mathayo 2:12-13 TKU

Lakini Mungu aliwaonya wenye hekima hao katika ndoto kuwa wasirudi tena kwa Herode. Hivyo kwa kutii walirudi nchini kwao kwa kupitia njia nyingine. Baada ya wenye hekima kuondoka, malaika wa Bwana akamjia Yusufu katika ndoto na kumwambia, “Damka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake ukimbilie Misri kwa sababu Herode amedhamiria kumwua mtoto na sasa atatuma watu kumtafuta. Na mkae Misri mpaka nitakapowaambia mrudi.”

Прочитати Mathayo 2