Mathayo 4
4
Yesu Ajaribiwa na Shetani
(Mk 1:12-13; Lk 4:1-13)
1Kisha Roho Mtakatifu akamwongoza Yesu hadi nyikani ili akajaribiwe na Shetani. 2Baada ya Yesu kufunga kwa siku arobaini mchana na usiku, akaumwa njaa sana. 3Mjaribu#4:3 Mjaribu Kwa maana ya kawaida, “Shetani”. akamwendea na akasema, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, basi yaamuru mawe haya yawe mikate.”
4Yesu akajibu, “Maandiko yanasema, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Mungu.’”#Kum 8:3
5Kisha Shetani alimwongoza Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerusalemu na akamweka juu ya mnara wa Hekalu. 6Akamwambia Yesu, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe mpaka chini! Kwani Maandiko yanasema,
‘Mungu atawaamuru malaika zake wakusaidie,
na mikono yao itakupokea,
ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’”#Zab 91:11-12
7Yesu akamjibu, “Pia, Maandiko yanasema, ‘usimjaribu Bwana Mungu wako.’”#Kum 6:16
8Kisha Shetani akamwongoza Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima ulio mrefu sana na kumwonyesha falme zote za ulimwengu na vitu vya kupendeza vilivyomo ndani. 9Shetani akamwambia Yesu, “Ukiinama na kuniabudu, nitakupa vitu hivi vyote.”
10Yesu akamjibu Shetani akamwambia, “Ondoka kwangu Shetani! Kwani Maandiko yanasema, ‘Umwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake!’”#Kum 6:13
11Baada ya hayo, Shetani akamwacha. Ndipo malaika wakaja kumhudumia.
Yesu Aanza Kazi yake Galilaya
(Mk 1:14-15; Lk 4:14-15)
12Yesu aliposikia kuwa Yohana alikuwa amefungwa gerezani, alirudi katika wilaya ya Galilaya. 13Lakini aliondoka Nazareti. Alikwenda kuishi Kapernaumu, mji ulio kando ya Ziwa Galilaya katika eneo la Zabuloni na Naftali. 14Hili lilitokea ili kutimiza maneno aliyosema nabii Isaya:
15“Sikilizeni, enyi nchi ya Zabuloni na Naftali,
nchi iliyo kando ya barabara iendayo baharini,
ng'ambo ya Mto Yordani!
Galilaya, wanapokaa Mataifa.
16Watu wanaoishi katika giza ya kiroho,
nao wameiona nuru iliyo kuu.
Nuru hiyo imeangaza kwa ajili yao wale
wanaoishi katika nchi yenye giza kama kaburi.”#Isa 9:1-2
17Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia watu ujumbe wake unaosema, “Mbadili mioyo yenu na maisha yenu pia, kwa sababu Ufalme wa Mungu umewafikia.”
Yesu Achagua Baadhi ya Wafuasi
(Mk 1:16-20; Lk 5:1-11)
18Yesu alipokuwa akitembea kando ya Ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni, aitwaye Petro na nduguye aitwaye Andrea. Ndugu hawa walikuwa wavuvi na walikuwa wanavua samaki kwa nyavu zao. 19Yesu akawaambia, “Njooni, mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa aina nyingine. Nitawafundisha jinsi ya kukusanya watu badala ya samaki.” 20Mara moja, Simoni na Andrea wakaziacha nyavu zao na kumfuata Yesu papo hapo.
21Yesu akaendelea kutembea kutoka pale. Akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo. Walikuwa kwenye mashua pamoja na Zebedayo baba yao. Walikuwa wakiandaa nyavu zao za kuvulia samaki. Yesu akawaita wamfuate. 22Mara moja wakaiacha mashua pamoja na baba yao na wakamfuata Yesu.
Yesu Afundisha na Kuponya Watu
(Lk 6:17-19)
23Yesu alikwenda sehemu zote za Galilaya, akifundisha na akihubiri Habari Njema katika masinagogi kuhusu Ufalme wa Mungu. Aliponya magonjwa yote na madhaifu mengi ya watu. 24Habari kuhusu Yesu zilienea katika nchi yote ya Shamu, na watu waliwaleta wale wote wenye kuteswa na magonjwa na maumivu mbalimbali. Baadhi yao walikuwa na mashetani, wengine walikuwa na kifafa na wengine walikuwa wamepooza. Yesu akawaponya wote. 25Makundi makubwa ya watu walimfuata; watu kutoka Galilaya, na jimbo lililoitwa Miji Kumi,#4:25 Miji Kumi Jimbo hili lilikuwa mashariki ya Ziwa la Galilaya na wakazi wake hawakuwa Wayahudi. Miji Kumi imejulikana pia kama Dekapoli. Yerusalemu, Yuda na maeneo ng'ambo ya Mto Yordani.
Поточний вибір:
Mathayo 4: TKU
Позначайте
Поділитись
Копіювати
Хочете, щоб ваші позначення зберігалися на всіх ваших пристроях? Зареєструйтеся або увійдіть
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Toleo la Awali
© 2017 Bible League International

: