Yohana Utangulizi

Utangulizi
Miongoni mwa Injili zote nne, Injili ya Yohana ni ya kipekee. Ingawa kwa ujumla inaonyesha maisha ya Yesu na huduma yake, Injili hii haina mifano. Ina miujiza miwili tu iliyoandikwa katika zile Injili nyingine, na miujiza mingine mitano ambayo ni Yohana peke yake aliyeielezea.
Mwandishi
Yohana mwana wa Zebedayo, nduguye Yakobo.
Kusudi
“Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake” (20:31).
Mahali
Uwezekano mkubwa ni kwamba Injili hii iliandikiwa Efeso.
Tarehe
Kama mwaka wa 85–90 B.K.
Wahusika Wakuu
Yesu, mama yake, na wanafunzi wake Yesu; Yohana Mbatizaji na wanafunzi wake; Maria, Martha na Lazaro; Pilato, wakuu wa dini ya Kiyahudi, na Maria Magdalene.
Wazo Kuu
Injili ya Yohana inatilia mkazo zaidi Uungu wa Kristo. Pia inatueleza kwa undani zaidi ishara ambazo Injili nyingine zinaziita miujiza, ili msomaji aweze kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, na kwamba mtu anaweza kupata uzima wa milele tu kwa kumwamini Yesu.
Mambo Muhimu
Katika Injili hii tunapata habari za baadhi ya miujiza ya Yesu, na mafundisho yake ambayo hayakutajwa katika Injili zingine. Sehemu ya sura 14–17 inaeleza mafundisho ambayo Yesu aliwapa wanafunzi wake kabla ya kifo chake. Sehemu nyingine inaeleza jinsi Yesu alivyojidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwake.
Mgawanyo
Yesu ni Mungu (1:1-14)
Huduma ya Yesu kabla ya kwenda Galilaya (1:15–4:54)
Huduma ya Yesu huko Galilaya, na upinzani uliomkabili huko Yerusalemu (5:1–10:42)
Kufufuliwa kwa Lazaro (11:1-57)
Kukamilishwa kwa huduma ya Bwana Yesu (12:1–13:38)
Mafundisho ya mwisho ya Bwana Yesu (14:1–17:26)
Kufa na kufufuka kwa Yesu (18:1–20:10)
Kuonekana kwa Yesu baada ya kufufuka (20:11–21:25).

Currently Selected:

Yohana Utangulizi: NEN

Qaqambisa

Share

Copy

None

Ufuna ukuba iimbalasane zakho zigcinwe kuzo zonke izixhobo zakho? Bhalisela okanye ngena