Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo mna upotovu, bali mjazwe Roho wa Mungu. Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana Isa mioyoni mwenu, siku zote mkimshukuru Mungu Baba Mwenyezi kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi.