1
1 Pet 2:9
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu
Compare
Explore 1 Pet 2:9
2
1 Pet 2:24-25
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.
Explore 1 Pet 2:24-25
3
1 Pet 2:10
ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.
Explore 1 Pet 2:10
4
1 Pet 2:2
Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu
Explore 1 Pet 2:2
5
1 Pet 2:11-12
Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Explore 1 Pet 2:11-12
6
1 Pet 2:5
Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
Explore 1 Pet 2:5
7
1 Pet 2:1
Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
Explore 1 Pet 2:1
8
1 Pet 2:4
Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
Explore 1 Pet 2:4
9
1 Pet 2:16
kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu.
Explore 1 Pet 2:16
10
1 Pet 2:15
Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu
Explore 1 Pet 2:15
Home
Bible
Plans
Videos